binti mdogo mjamzito kimedhaminiwa na google |
Maisha ya ufukura imesababishia vifo vya watoto wengi kabla ya kuzaliwa au hata wakati au baada ya kuzaliwa. Hata ingawa maisha ya wanawake wajawazito imezidi kuboreshwa, kupitia uanzilishi wa 'Linda Mama Boresha Jamii," inayotoa huduma za bure kwa kina mama waja wazito katika hospitali za serikali, huduma hizi hazisaidii aslilimia mia ya wanawake. Suluhisho la asilimia mia ni lipi? sidhani nina jibu, ila nawasikitia kina mama ambao wanakumbana na shida hizi, kwani wengi pia hupoteza maisha yao hasa wakati wa kujifungua.
Iwapo wewe ni mzaliwa wa jijini, shukuru Mungu. Iwapo eneo lenu au hata bara kwenu kuna hospitali, na huduma zinapatikana kwa urahisi, basi wewe ni mmoja wapo wa wale wenye bahati nasibu. Tunao adinasi wengi wanaoishi katika maeneo ya kusikitisha sana. baadhi ya maeneo haya ni kama vile sehemu nyingi za kaskazini mashariki. Eneo hizi zina hospitali chache sana za serikali na barabara pia ni duni ajabu, hivyo kuwasababishia wanaoishi mbali kushindwa kufika hospitalini ili kupata matibabu. Je, tatizo hili laweza kutatuliwa na nani kama si serikali? Ahadi tunazo, lakini ngoja ngoja itazidi kutuumiza matumbo, huku watoto wengi wakikaribishwa duniani na kifo.
Mama mja mzito anapaswa kuenda hospitalini takriban kila mwezi ili kuangaliwa iwapo kitoto chake tumboni kinakua salama salimini, au iwapo ana ugonjwa wowote ili kuelekezwa ipasavyo. Katika maeneo ambayo hospitali ni chache na kuna ugumu wa kuyatembelea kutokana na umbali na barabara mbovu, wanawake wengi huamua kuwatembelea wakunga wenye ujuzi ili wasaidike. Wakunga hawa hutumia miti shamba kutokana na itikadi zao za kitamaduni. Mbinu hizi huhatarisha maisha ya mama pamoja na kitoto chake tumboni na hivyo huchangia pakubwa katika vifo vya mama wajawazito au watoto wachanga. Na hivi ndivyo wanavyo karibishwa duniani baadhi ya wana wetu.
Hiki ni kilio, hiki ni kilio changu na natumai pia ya wale wenye macho ya kuweza kuyaona niyaonayo mimi. kwenye mizani, sijui waweza kuipa serikali uzito upi katika kuangalia maslahi ya kina mama waja wazito, hasa katika haya maeneo duni yaliyojaa walala hoi, wale tuwaitao 'maskini hohehahe.' ?
Mama mja mzito anapaswa kuenda hospitalini takriban kila mwezi ili kuangaliwa iwapo kitoto chake tumboni kinakua salama salimini, au iwapo ana ugonjwa wowote ili kuelekezwa ipasavyo. Katika maeneo ambayo hospitali ni chache na kuna ugumu wa kuyatembelea kutokana na umbali na barabara mbovu, wanawake wengi huamua kuwatembelea wakunga wenye ujuzi ili wasaidike. Wakunga hawa hutumia miti shamba kutokana na itikadi zao za kitamaduni. Mbinu hizi huhatarisha maisha ya mama pamoja na kitoto chake tumboni na hivyo huchangia pakubwa katika vifo vya mama wajawazito au watoto wachanga. Na hivi ndivyo wanavyo karibishwa duniani baadhi ya wana wetu.
mama mjamzito katika eneo duni. kimedhaminiwa na google |
Sote ni waathiriwa kwa njia moja au nyingine, kina mama hawa ni jamaa zetu. Sio tu katika maeneo haya, bali nchi nzima inakumbana na shida nyingi katika kuwahudumia kina mama wajawazito. Ufisadi uongozini umekithiri mipaka na kuzorotesha utoaji huduma. Leo hii, idadi ya kina mama katika wadi za kujifungua imeongezeka maradufu, ilhali vifaa ni vile vile(vichache mno). Dawa hazipatikani hospitalini na mara nyingi wagonjwa hulazima kununua dawa katika maduka ya dawa ambayo sana sana zinamilkiwa na wahudumu wa hospitalini, hasa madaktari wenye vyeo kubwa kubwa. Ndiyo huduma ya bure hii, au vipi?
Heko kina mama wote! nawavulieni kofia kwa mengi magumu mliyoyapitia ili kuwafikisha wana duniani. bila shaka tumeijaza alivyoamuru Mwenyezi Mungu. Shukuru ulivyopokelewa duniani, maana ni wengi dunia hii waliionea paa!

karibu duniani. kimedhaminiwa na google. |
No comments:
Post a Comment