Siku nenda siku rudi, tunashuhudia sakata ya makali ya kiangazi na njaa nchini pasi na matumaini ya kupata suluhisho la kudumu. Vyombo vya habari hutupa taswira ya kutamausha kwa kuangazia swala nyeti la kiangazi na baa la njaa. Ni utu au uhayawani, tunapowakodolea macho kodo waathiriwa wa njaa huku tukila na kusaza?
Wana nyuso za kusikitisha, miili yao iliyokonda na kukondeana pia ni ya kughadhabisha, lakini nani wa kuwasaidia? Lisilobudi hubidi, na wao hawana budi ila kuamka kila uchao na kupambana na hali yao huku wakiwa na matumaini ya kupata afueni katika siku za usoni au kupitia kwa wasamaria wema. Huenda siku moja Maulana atafanya miujizi na masaibu wanayopitia waja hawa yatatokomea milele, kwani serikali inayopaswa kuwajali, haijali togo wala jando. Ni wengi wamepoteza maisha yao, na kuwa kitoweo cha mauti, kwa ukosefu wa chakula. La haula!, sheria ya maskini haiko katika serikali ya mwenye navyo.
Mashirika yasiyo ya kiserikali alimaarufu (NGO's) kwa lugha ya kimombo, yamekuwa katika mstari wa mbele kwa kusaidia mikasa kama hii. Mashirika haya ambayo sana sana huwategemea wasamaria wema ili kutoa misaada yao, hujizatiti mno kwa kutoa huduma zao. Juhudi ambazo iwapo serikali ingeweza kuiga, basi majanga kama haya yangekuwa nadra sana. Cha kusikitisha ni kuwa, serikali ina uwezo mkubwa wa kuwasaidi maskini hohehahe hapa nchini, zaidi ya mashirika haya ya kibinafsi, ila ubinafsi na ufisadi uongozini, umesababishia kuwasahau wahusika wakuu wanaohitaji fedha za serikali.
Kila mwaka, bajeti inapotolewa, pesa hutengwa kwa mikakati ya sekta mbalimbali serikalini. Pesa hizi ni pamoja na pesa za kusaidia kukabiliana na majanga kama haya ya njaa na ukame nchini. Swali ni je, pesa hizi hutimiza kazi zilizokusudiwa au huishia mifukoni mwa watu binafsi?
Viongozi wetu wanapotoa misaada kwa majanga kama haya, wao huyafanya yaoneka kana kwamba ni jambo la kustaajabisha au kuvuliwa kofia. Wengi hujipigia debe na kujipiga kifua ili waonekane wachapa kazi, lakini ukweli ni kuwa, sivyo tudhaniavyo sisi. Katika asilimia mia ya pesa wanazopewa kuwasaidia watu mashinani, aslimia zaidi huishia katika mifuko yao. Kiwango cha msaada wanaotoa ni kidogo ghaya, na wakati wanapotoa wao huandamana na wanahabari na kujaza picha mitandaoni ili kuanikia wakenye jinsi walivyo wachapa kazi, ukweli ukiwa ni kinyume. Msaada wa hakika hauhitaji matangazo, sio lazima ugonge vichwa vya habari ndio uonekane kama msaada, kumbuka zuri chajiuza, kibaya chajitembeza.
Waswahili walinena kuwa, tenda wema nenda zako, wakaja wakaongeza kuwa, wema hauozi, lakini wema wa serikali yetu pamoja na uongozi wake ni wema wa aina gani? Ni wema huu, au uozo na unyama? Mtu mwenye akili timamu na mwenye utu ya binadamu anaweza kuwakodolea macho watu wanaokufa kutokana na njaa, ilhali pesa zinazostahili kuwasaidia, anajilimbikizia na kujiendelezea utajiri? Si huu ndio uhayawani aliyoimba msanii Nyashinski? Si haki kabisa!
Ukweli mtupu, serikali should put in some extra effort... Nimeshindwa kucomment in pure swahili 😂😂
ReplyDeleteKABISAAAA
DeleteNilipambana na utasa kwa miaka mingi hadi mwishowe nikakata tamaa. Lakini kama msemo unavyoenda, kuna marafiki ambao haukutani mara mbili maishani. Shukrani kwa rafiki mzuri sana ambaye alinitambulisha kwa Dk. Dawn, kila kitu kilibadilika.
ReplyDeleteBaada ya kueleza hali yangu, Dk. Dawn aliahidi kunisaidia katika tambiko la ujauzito. Kusema kweli, sikuamini kwamba ingefaa kwa sababu tayari nilikuwa na umri wa miaka 40, lakini niliamua kufuata maagizo. Kwa mshangao mkubwa, wiki tatu tu baadaye, nilipata mimba!
Furaha iliyokuwa moyoni mwangu—na katika mioyo ya mume wangu na familia—ilizidi kudhibitiwa nilipowaonyesha matokeo chanya ya ujauzito. Baadaye nilijifungua salama na kwa amani, na baada ya mwaka mmoja na miezi minane, nilipata mimba tena. Hakika ulikuwa ni muujiza usioelezeka.
Tangu wakati huo, nimependekeza Dk. Dawn kwa wanawake wengine wengi, na matokeo yao pia yamekuwa kama ilivyotarajiwa. Ndiyo maana ninapendekeza kwa moyo wote Dk. Dawn kwa mwanamke yeyote anayehangaika na utasa, matatizo ya ndoa au uhusiano, magonjwa, au aina yoyote ya suala la kiroho. Hakika atatoa suluhisho la kudumu.
📞 WhatsApp: +2349046229159
🌹 Ushuhuda Wangu Kuhusu Dkt. Dawn – Mtu Aliyerejesha Nyumba Yangu na Furaha Yangu
ReplyDeleteNataka kushiriki ushuhuda wangu wa dhati kuhusu jinsi Dkt. Dawn alivyobadilisha maisha yangu kabisa.
Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na alikuwa ameenda kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.
Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwangu — na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.
Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.
Lakini si hayo tu — Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyokuwa ikizunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.
Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote — huzuni, bahati mbaya, au mkanganyiko — usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.
Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.co