Wednesday, 25 April 2018

LULU HASSAN

Siulize Ni kwa Nini, Nam enzi huyu Lulu
Ueledi wake Shani, taka iga nifaulu
Kwenye lugha namba wani, uliza hadi ikulu
Mwanahabari shupavu, Siri yako fichulie

Kitizama likotoka, hatua mepiga Sana
Katika vyombo tajika, kazi yako tumeona
Citizeni bila Shaka, wapambia kama hina
Mwanahabari shupavu, Siri yako fichulie.

Sauti yako nyororo, Kama chatu navutiwa
Katika giza totoro, niondowe Kama njiwa
Wanionao kiporo, Washtuke kipakuliwa
Mwanahabari shupavu, Siri yako fichulie.

Taka huo ujasiri, taka huo ubunifu
Kwenye kamera si siri, kazi ngumu ya kusifu
Nataka kuwa mahiri, Kama wewe mkufuu
Mwanahabari shupavu, Siri yako fichulie.

Tafurahi kitimiza, ndoto yangu aushini
Ninaapa kutocheza, funzo lako tathamini
Niinue Kama pweza, nyayo zako natamani
Mwanahabari shupavu, Siri yako fichulie.

Lulu jina Kama ua, nipambie ari yangu
Hasani mama tambua, taka uwe ngao yangu
Maza Aziza najua, kazi zako hizi tangu
Mwanahabari shupavu, Siri yako fichulie.

Natumai mesikia, ombi langu la moyoni
Siriyo natamania, ila bado ni taabani
Kama vile abiria,  lako gari niko ndani
Mwanahabari shupavu, Siri yako fichulie.
Lulu Hassan.

1 comment:

  1. Nilipambana na utasa kwa miaka mingi hadi mwishowe nikakata tamaa. Lakini kama msemo unavyoenda, kuna marafiki ambao haukutani mara mbili maishani. Shukrani kwa rafiki mzuri sana ambaye alinitambulisha kwa Dk. Dawn, kila kitu kilibadilika.

    Baada ya kueleza hali yangu, Dk. Dawn aliahidi kunisaidia katika tambiko la ujauzito. Kusema kweli, sikuamini kwamba ingefaa kwa sababu tayari nilikuwa na umri wa miaka 40, lakini niliamua kufuata maagizo. Kwa mshangao mkubwa, wiki tatu tu baadaye, nilipata mimba!

    Furaha iliyokuwa moyoni mwangu—na katika mioyo ya mume wangu na familia—ilizidi kudhibitiwa nilipowaonyesha matokeo chanya ya ujauzito. Baadaye nilijifungua salama na kwa amani, na baada ya mwaka mmoja na miezi minane, nilipata mimba tena. Hakika ulikuwa ni muujiza usioelezeka.

    Tangu wakati huo, nimependekeza Dk. Dawn kwa wanawake wengine wengi, na matokeo yao pia yamekuwa kama ilivyotarajiwa. Ndiyo maana ninapendekeza kwa moyo wote Dk. Dawn kwa mwanamke yeyote anayehangaika na utasa, matatizo ya ndoa au uhusiano, magonjwa, au aina yoyote ya suala la kiroho. Hakika atatoa suluhisho la kudumu.

    📞 WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete

LULU HASSAN

Siulize Ni kwa Nini, Nam enzi huyu Lulu Ueledi wake Shani, taka iga nifaulu Kwenye lugha namba wani, uliza hadi ikulu Mwanahabari shupavu...