Kikumbuka likotoka, mie chozi lanilenga
Japo mimba lipachika, kulikuza kajitenga
Muda bado, alimaka, tulitoe aliunga
Asante kwa Maulana, tatu mwaka tumefika.
Kwangu likuwa zawadi, kwa dhati lisubiria
Japo shida ilizidi, Kwa Mola liangazia,
Uzazi kwangu libidi, Hata shule kuachia
Asante kwa Maulana, tatu mwaka tumefika.
Ni mbali kifikiria, tumetoka na mwanangu
Hata njaa kilalia, kwa kuzongwa na machungu
Ma' mkwe kasaidia, pokea shukrani zangu
Asante kwa Maulana, tatu mwaka tumefika.
Mwana ukizidi kua, mema mengi zingatia
Heshima kwako tambua, kote kote angazia
Wako baba keshajua, ndiwe wake malkia
Asante kwa Maulana, tatu mwaka tumefika.
Japo baba nami mama, kisogo lishapeana
Kwako mwana tulisema, takulea kwa kufana
Hakikisho la kusoma, tatimiza na kwa sana
Asante kwa Maulana, tatu mwaka tumefika.
Sasa natia kikomo, tamati ya simulizi
Mwana menipa kisomo, cha maisha wazi wazi
Tatu mwaka siwe shimo, mengi mema na yazidi
Asante kwa Maulana, tatu mwaka tumefika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
LULU HASSAN
Siulize Ni kwa Nini, Nam enzi huyu Lulu Ueledi wake Shani, taka iga nifaulu Kwenye lugha namba wani, uliza hadi ikulu Mwanahabari shupavu...
-
Azizi Ni kipusa aliyezaliwa na kulelewa kwa njia ya kipekee. Binti huyu mwenye maumbile ya kupendeza na sura nzuri alivutia wengi, wa karib...
-
Katika huzuni twaomboleza, katika huruma tumefarijiwa sisi tuliyofiwa. Tuko makuburini ambapo kanisa, ndugu na jamaa wameungana nasi ili kum...
-
"Sabrina! Sabrina! Fungua tafadhali! Mwanangu fungua tuyazungumzie." Babangu anayakatisha mawazo yangu huku akiubisha mlango kwa f...
No comments:
Post a Comment